11 Nilipofanya gunia kuwa nguo zangu,Nikawa mithali kwao.
12 Waketio langoni hunisema,Na nyimbo za walevi hunidhihaki.
13 Nami maombi yangu nakuomba Wewe, BWANA,Wakati ukupendezao; Ee Mungu,Kwa wingi wa fadhili zako unijibu,Katika kweli ya wokovu wako.
14 Uniponye kwa kunitoa matopeni,Wala usiniache nikazama.Na niponywe nao wanaonichukia,Na katika vilindi vya maji.
15 Mkondo usinigharikishe, wala vilindi visinimeze,Wala shimo lisifumbe kinywa chake juu yangu.
16 Ee BWANA, unijibu, maana fadhili zako ni njema,Kwa kadiri ya rehema zako unielekee.
17 Wala usinifiche uso wako, mimi mtumishi wako,Maana mimi nimo taabuni, unijibu upesi.