19 Wewe umejua kulaumiwa kwangu,Na kuaibika na kufedheheka kwangu,Mbele zako Wewe wako watesi wangu wote.
20 Laumu imenivunja moyo,Nami ninaugua sana.Nikangoja aje wa kunihurumia, wala hakuna;Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu.
21 Wakanipa uchungu kuwa chakula changu;Nami nilipokuwa na kiu wakaninywesha siki.
22 Meza yao mbele yao na iwe mtego;Naam, wakiwa salama na iwe tanzi.
23 Macho yao yatiwe giza wasione,Na viuno vyao uvitetemeshe daima.
24 Uimwage ghadhabu yako juu yao,Na ukali wa hasira yako uwapate.
25 Matuo yao na yawe ukiwa,Pasiwe na mtu wa kukaa hemani mwao.