5 Ee Mungu, unajua upumbavu wangu,Wala hukufichwa dhambi yangu.
6 Wanaokungoja Wewe wasiaibishwe,Kwa ajili yangu, Bwana, MUNGU wa majeshi.Wanaokutafuta Wewe wasifedheheshwe,Kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli.
7 Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu,Fedheha imenifunika uso wangu.
8 Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu,Na msikwao kwa wana wa mama yangu.
9 Maana wivu wa nyumba yako umenila,Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata.
10 Nilipolia na kuiadhibu roho yangu kwa kufunga,Ikawa laumu juu yangu.
11 Nilipofanya gunia kuwa nguo zangu,Nikawa mithali kwao.