1 Nimekukimbilia Wewe, BWANA,Nisiaibike milele.
2 Kwa haki yako uniponye, uniopoe,Unitegee sikio lako, uniokoe.
3 Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu,Nitakakokwenda sikuzote.Umeamuru niokolewe,Ndiwe genge langu na ngome yangu.
4 Ee Mungu wangu, uniopoe mkononi mwa mkorofi,Katika mkono wake mwovu, mdhalimu,
5 Maana ndiwe taraja langu, Ee Bwana MUNGU,Tumaini langu tokea ujana wangu.