3 Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu,Nitakakokwenda sikuzote.Umeamuru niokolewe,Ndiwe genge langu na ngome yangu.
4 Ee Mungu wangu, uniopoe mkononi mwa mkorofi,Katika mkono wake mwovu, mdhalimu,
5 Maana ndiwe taraja langu, Ee Bwana MUNGU,Tumaini langu tokea ujana wangu.
6 Nimekutegemea Wewe tangu kuzaliwa,Ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama yangu,Ninakusifu Wewe daima.
7 Nimekuwa kitu cha ajabu kwa watu wengi,Na Wewe ndiwe kimbilio langu la nguvu.
8 Kinywa changu kitajazwa sifa zako,Na heshima yako mchana kutwa.
9 Usinitupe wakati wa uzee,Nguvu zangu zipungukapo usiniache.