6 Maana siko mashariki wala magharibi,Wala nyikani itokako heshima.
7 Bali Mungu ndiye ahukumuye;Humdhili huyu na kumwinua huyu.
8 Maana mkononi mwa BWANA mna kikombe,Na mvinyo yake inatoka povu;Kumejaa machanganyiko;Naye huyamimina.Na sira zake wasio haki wa duniaWatazifyonza na kuzinywa.
9 Bali mimi nitatangaza matendo yako milele,Nitamwimbia Mungu wa Yakobo.