1 Enyi watu wangu, sikilizeni sheria yangu,Tegeni masikio kwa maneno ya kinywa changu.
2 Na nifunue kinywa changu kwa mithali,Niyatamke mafumbo ya kale.
3 Mambo tuliyoyasikia na kuyafahamu,Ambayo baba zetu walituambia.
4 Hayo hatutawaficha wana wao,Huku tukiwaambia kizazi kingine,Sifa za BWANA, na nguvu zake,Na mambo yake ya ajabu aliyoyafanya.
5 Maana alikaza ushuhuda katika Yakobo,Na sheria aliiweka katika Israeli.Aliyowaamuru baba zetuWawajulishe wana wao,
6 Ili kizazi kingine wawe na habari,Ndio hao wana watakaozaliwa.Wasimame na kuwaambia wana wao
7 Wamwekee Mungu tumaini lao.Wala wasiyasahau matendo ya Mungu,Bali wazishike amri zake.