19 Naam, walimwamba Mungu, wakasema,Je! Mungu aweza kuandika meza jangwani?
20 Tazama, aliupiga mwamba;Maji yakabubujika, ikafurika mito.Pia aweza kutupa chakula?Atawaandalia watu wake nyama?
21 Hivyo BWANA aliposikia akaghadhibika;Moto ukawashwa juu ya Yakobo,Hasira nayo ikapanda juu ya Israeli.
22 Kwa kuwa hawakumwamini Mungu,Wala hawakuutumainia wokovu wake.
23 Lakini aliyaamuru mawingu juu;Akaifungua milango ya mbinguni;
24 Akawanyeshea mana ili wale;Akawapa nafaka ya mbinguni.
25 Mwanadamu akala chakula cha mashujaa;Aliwapelekea chakula cha kuwashibisha.