6 Ili kizazi kingine wawe na habari,Ndio hao wana watakaozaliwa.Wasimame na kuwaambia wana wao
7 Wamwekee Mungu tumaini lao.Wala wasiyasahau matendo ya Mungu,Bali wazishike amri zake.
8 Naam, wasiwe kama baba zao,Kizazi cha ukaidi na uasi.Kizazi kisichojitengeneza moyo,Wala roho yake haikuwa amini kwa Mungu.
9 Wale Waefraimu, wenye silaha, wapiga upinde,Walirudi nyuma siku ya vita.
10 Hawakulishika agano la Mungu;Wakakataa kuenenda katika sheria yake;
11 Wakayasahau matendo yake,Na mambo yake ya ajabu aliyowaonyesha.
12 Mbele ya baba zao alifanya mambo ya ajabu,Katika nchi ya Misri, konde la Soani.