1 Maskani zako zapendeza kama nini,Ee BWANA wa majeshi!
2 Nafsi yangu imezionea shauku nyua za BWANA,Naam, na kuzikondea.Moyo wangu na mwili wanguVinamlilia Mungu aliye hai.
3 Shomoro naye ameona nyumba,Na mbayuwayu amejipatia kioto,Alipoweka makinda yake,Kwenye madhabahu zako, Ee BWANA wa majeshi,Mfalme wangu na Mungu wangu.
4 Heri wakaao nyumbani mwako,Wanakuhimidi daima.
5 Heri ambaye nguvu zake zatoka kwako,Na njia ziendazo Sayuni zimo moyoni mwake.
6 Wakipita kati ya bonde la Vilio,Hulifanya kuwa chemchemi,Naam, mvua ya vuli hulivika baraka
7 Huendelea toka nguvu hata nguvu,Huonekana Sayuni kila mmoja mbele za Mungu.