7 Maana tumetoweshwa kwa hasira yako,Na kwa ghadhabu yako tumefadhaishwa.
8 Umeyaweka maovu yetu mbele zako,Siri zetu katika mwanga wa uso wako.
9 Maana siku zetu zote zimepita katika hasira yako,Tumetowesha miaka yetu kama kite.
10 Siku za miaka yetu ni miaka sabini,Na ikiwa tuna nguvu miaka themanini;Na kiburi chake ni taabu na ubatili,Maana chapita upesi tukatokomea mara.
11 Ni nani aujuaye uweza wa hasira yako?Na ghadhabu yako kama ipasavyo kicho chako?
12 Basi, utujulishe kuzihesabu siku zetu,Tujipatie moyo wa hekima.
13 Ee BWANA urudi, hata lini?Uwahurumie watumishi wako.