20 Uniponye nafsi yangu na upanga,Mpenzi wangu na nguvu za mbwa.
21 Kinywani mwa simba uniokoe;Naam, toka pembe za nyati umenijibu.
22 Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu,Katikati ya kusanyiko nitakusifu.
23 Ninyi mnaomcha BWANA, msifuni,Enyi nyote mlio wazao wa Yakobo, mtukuzeni,Mcheni, enyi nyote mlio wazao wa Israeli.
24 Maana hakulidharau teso la mteswa,Wala hakuchukizwa nalo;Wala hakumficha uso wake,Bali alipomlilia akamsikia.
25 Kwako zinatoka sifa zanguKatika kusanyiko kubwa.Nitaziondoa nadhiri zanguMbele yao wamchao.
26 Wapole watakula na kushiba,Wamtafutao BWANA watamsifu;Mioyo yenu na iishi milele.