24 Maana hakulidharau teso la mteswa,Wala hakuchukizwa nalo;Wala hakumficha uso wake,Bali alipomlilia akamsikia.
25 Kwako zinatoka sifa zanguKatika kusanyiko kubwa.Nitaziondoa nadhiri zanguMbele yao wamchao.
26 Wapole watakula na kushiba,Wamtafutao BWANA watamsifu;Mioyo yenu na iishi milele.
27 Miisho yote ya dunia itakumbuka,Na watu watamrejea BWANA;Jamaa zote za mataifa watamsujudia.
28 Maana ufalme una BWANA,Naye ndiye awatawalaye mataifa.
29 Wakwasi wote wa dunia watakula na kusujudu,Humwinamia wote washukao mavumbini;Naam, yeye asiyeweza kujihuisha nafsi yake,
30 Wazao wake watamtumikia.Zitasimuliwa habari za BWANA,Kwa kizazi kitakachokuja,