1 Ee BWANA, nitakuita Wewe, mwamba wangu,Usiwe kwangu kama kiziwi.Nisije nikafanana nao washukao shimoni,Ikiwa umeninyamalia.
2 Uisikie sauti ya dua yangu nikuombapo,Nikipainulia patakatifu pako mikono yangu.
3 Usinikokote pamoja na wasio haki,Wala pamoja na watenda maovu.Wawaambiao jirani zao maneno ya amani,Lakini mioyoni mwao mna madhara.
4 Uwape sawasawa na vitendo vyao,Na kwa kadiri ya ubaya wa kufanya kwao,Uwape sawasawa na kazi ya mikono yao,Uwalipe stahili zao.