11 Kwa sababu ya watesi wangu nimekuwa laumu,Naam, hasa kwa jirani zangu;Na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu;Walioniona njiani walinikimbia.
12 Nimesahauliwa kama mfu asiyekumbukwa;Nimekuwa kama chombo kilichovunjika.
13 Maana nimesikia masingizio ya wengi;Hofu ziko pande zote.Waliposhauriana juu yangu,Walifanya hila wauondoe uhai wangu.
14 Lakini mimi nakutumaini Wewe, BWANA,Nimesema, Wewe ndiwe Mungu wangu.
15 Nyakati zangu zimo mikononi mwako;Uniponye na adui zangu, nao wanaonifuatia.
16 Umwangaze mtumishi wakoKwa nuru ya uso wako;Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.
17 Ee BWANA, nisiaibishwe, maana nimekuita;Waaibishwe wasio haki, wanyamaze kuzimuni.