1 Nalimngoja BWANA kwa saburi,Akaniinamia akakisikia kilio changu.
2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu,Toka udongo wa utelezi;Akaisimamisha miguu yangu mwambani,Akaziimarisha hatua zangu.
3 Akatia wimbo mpya kinywani mwangu,Ndio sifa zake Mungu wetu.Wengi wataona na kuogopa,Nao watamtumaini BWANA
4 Heri aliyemfanya BWANA kuwa tumaini lake,Wala hakuwaelekea wenye kiburi,Wala hao wanaogeukia uongo.