11 Nawe, BWANA, usinizuilie rehema zako,Fadhili zako na kweli yako na zinihifadhi daima.
12 Kwa maana mabaya yasiyohesabikaYamenizunguka mimi.Maovu yangu yamenipata,Wala siwezi kuona.Yamezidi kuliko nywele za kichwa changu,Na moyo wangu umeniacha.
13 Ee BWANA, uwe radhi kuniokoa,Ee BWANA, unisaidie hima.
14 Waaibike, wafedheheke pamoja,Wanaoitafuta nafsi yangu waiangamize.Warudishwe nyuma, watahayarishwe,Wapendezwao na shari yangu.
15 Wakae hali ya ukiwa, na iwe aibu yao,Wanaoniambia, Ewe! Ewe!
16 Washangilie, wakufurahie,Wote wakutafutao.Waupendao wokovu wakoWaseme daima, Atukuzwe BWANA.