4 Heri aliyemfanya BWANA kuwa tumaini lake,Wala hakuwaelekea wenye kiburi,Wala hao wanaogeukia uongo.
5 Ee BWANA, Mungu wangu, umefanya kwa wingiMiujiza yako na mawazo yako kwetu;Hakuna awezaye kufananishwa nawe;Kama ningependa kuyatangaza na kuyahubiri,Ni mengi sana hayahesabiki.
6 Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo,Masikio yangu umeyazibua,Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka.
7 Ndipo niliposema, Tazama nimekuja,(Katika gombo la chuo nimeandikiwa,)
8 Kuyafanya mapenzi yako,Ee Mungu wangu, ndiyo furaha yangu;Naam, sheria yako imo moyoni mwangu.
9 Nimehubiri habari za haki katika kusanyiko kubwa.Sikuizuia midomo yangu; Ee BWANA, unajua.
10 Sikusitiri haki yako moyoni mwangu;Nimetangaza uaminifu wako na wokovu wako.Sikuficha fadhili zako wala kweli yakoKatika kusanyiko kubwa.