13 Uwakomeshe kwa hasira,Uwakomeshe watoweke,Wajue ya kuwa Mungu atawala katika Yakobo,Na hata miisho ya dunia.
14 Wakati wa jioni hurudi, hulia kama mbwa,Na kuzunguka-zunguka mjini.
15 Watatanga-tanga hao wakitafuta chakula;Wasiposhiba watakesha usiku kucha.
16 Nami nitaziimba nguvu zako asubuhi,Nitaziimba fadhili zako kwa furaha.Kwa kuwa ndiwe uliyekuwa ngome yangu,Na makimbilio siku ya shida yangu.