1 Ee Mungu, uniokoe,Maana maji yamefika mpaka nafsini mwangu.
2 Ninazama katika matope mengi,Pasipowezekana kusimama.Nimefika penye maji ya vilindi,Mkondo wa maji unanigharikisha.
3 Nimechoka kwa kulia kwangu,Koo yangu imekauka.Macho yangu yamedhoofuKwa kumngoja Mungu wangu.
4 Wanaonichukia bure ni wengiKuliko nywele za kichwa changu.Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari,Adui zangu kwa sababu isiyo kweli.Hata mimi nalilipishwa kwa nguvuVitu nisivyovichukua.