1 Nalimngoja BWANA kwa saburi,Akaniinamia akakisikia kilio changu.
2 Akanipandisha toka shimo la uharibifu,Toka udongo wa utelezi;Akaisimamisha miguu yangu mwambani,Akaziimarisha hatua zangu.
3 Akatia wimbo mpya kinywani mwangu,Ndio sifa zake Mungu wetu.Wengi wataona na kuogopa,Nao watamtumaini BWANA
4 Heri aliyemfanya BWANA kuwa tumaini lake,Wala hakuwaelekea wenye kiburi,Wala hao wanaogeukia uongo.
5 Ee BWANA, Mungu wangu, umefanya kwa wingiMiujiza yako na mawazo yako kwetu;Hakuna awezaye kufananishwa nawe;Kama ningependa kuyatangaza na kuyahubiri,Ni mengi sana hayahesabiki.
6 Dhabihu na matoleo hukupendezwa nazo,Masikio yangu umeyazibua,Kafara na sadaka za dhambi hukuzitaka.
7 Ndipo niliposema, Tazama nimekuja,(Katika gombo la chuo nimeandikiwa,)